Kauli mbiu ya Juma la Kimataifa la Uwazi wa Kupata Machapisho ya Kitaaluma 2023: Jamii Kuelekea Ubwasharishaji

“Jamii Kuelekea Ubwasharishaji” ni kauli mbio ya ya Juma la Kimataifa la Uwazi wa Kupata Machapisho ya Kitaaluma inayoadhimishwa mwezi Oktoba 23-29 mwaka huu 2023: Kauli mbiu hii inalenga kuchochea mazungumzo ya dhati kuhusu njia ambazo uwazi wa kitaaluma unatoa kipaumbele matakwa ya wananchi na jamii ya wanatalaama- na ambazo hazitoi kipaumbele kwa makundi haya.

Nchi 193 wanachama wa shirika la elimu dunia lijulikanalo kama UNESCO ziliridhia azimio la Uwazi wa Sayansi (Open Science) ambalo linatoa kipaumbele kwa “Jamii Kuelekea Ubwasharishaji” zikitoa wito wa “kuzuia uvunaji usiokua sawia wa faida ipatikanayo kutokana na shughuliza za tafiti zitokanazo na ufadhiri wa fedha ya umma” na kuunga mkono muundo wa uchapishaji usiokua wa kiabiashara na muundo wa mashilikiano katika uchapishaji usio kuwa na gharama mchakato wa uchapishaji wa makala. Tukilenga maeneo haya tunaweza kufanikiwa kufikia maono halisi ambayo uwazi katika uchapishaji wa kitaaluma uliyaweka tangu mwanzo: Utamaduni wa kizamani na tekinolojia ya kisasa vimeungana kuleta uwezekano usiokua wa kawaida kwa manufaa ya umma.

Pale ambapo matakwa ya kibiashara yanapewa kipaumbele kuliko yale ya jamii ambayo utafiti ndiyo unalenga kuyafikia, mambo mengi yanajitokeza. Juma la kimataifa la uwazi wa machapisho ya kibiashara unatoa fursa kwa mtu mmoja mmoja kuzungumzia masuala ambayo ni msingi katika mazingira yao. Masuala haya yanaweza kuhusisha: Nini kinapotea pale ambapo idadi inayopungua ya mashirika yanamiliki uzailishaji wa maarifa badala ya watafiti wenyewe? Nini gharama ya muundo wa kibiashara ambao unajikita zaidi katika kulimbikiza faida? Ni katika kipindi kipi ambao uwazi wa ukusanyaji na utumiaji wa data za mtafiti zinaweza kufifisha uhuru wa kitaaluma? Je,kuna uwezekano wa ubiasharishaji kusaidia matakwa ya umma? Kuna miundo mbinu ipi ambayo iko ndani ya uwezo wa jamii na inaweza kutumika kusaidia matakwa ya jumuia ya watafiti na jamii (mfano kanzidata za rasimu za makala, vihenge, na mifumo ya uchapishaji wa wazi?) Namna gani tunaweza kuhamisha mazoea kuelekea utumiaji wa  njia hizi ambazo jamii inazihitaji?

 

Kauli mbiu iliyochaguliwa na Kamati ya Ushauri ya Juma la Uwazi wa Kupata Machapisho ya kitaaluma ya mwaka huu inatoa fursaha ya kuungana pamoja, kuchukua hatua, na kutoa uelewa katika umuhimu wa kusimamia mifumo ya usambazaji wa maarifa. Juma la Uwazi wa Kupata Machapisho ya kitaaluma 2023 litaadhimishwa tarehe 23 mpaka 29 Oktoba; Hata hivyo, yeyote anahimizwa kukarimisha mijadala na kuchukua hatua kadri inavyowezekana ndani ya mwaka na kuichukua kauli mbiu na kazi mbalimbali kulingana na mazingira ya mahali husika.

Kwa taarifa kuhusu Juma la Uwazi wa Kupata Machapisho ya kitaaluma, tafadhari tembelea openaccessweek.org. twitter ya kiofisi, hastag ya juma ni #OAWeek.

Tafsiri ya tangazo hili katika lugha zingine zinaweza kupatikana katika openaccessweek.org.

Michoro kwa ajili ya Juma la Uwazi wa Kupata Machapisho ya kitaaluma inapatikana hapa openaccessweek.org.

[Translated by: Paul Muneja ]

Previous
Previous

Kiswahili (Kenyan)

Next
Next

বাংলা